Simba SC leo wametoa zawadi kwa mfadhili wao Mohamed Dewji baada ya kupata ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Stand United katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliopigwa kwenye Dimba la Taifa Dar es Salaam. Mabao ya Simba kwenye mchezo wa leo yamefungwa na Clatous Chama dakika ya 31, Emmanuel Okwi dakika ya 45 na bao la kujifunga kupitia kwa Eric Mulilo dakika ya 78. Simba inapata ushindi huo ikiwa ni siku tangu mfanyabiashara huyo kupatikana baada ya kutekwa tangu Oktoba 11 mwaka huu. Haya hapa mabao yenyewe.