Content removal request!


Goli: Singida United walivyotandikwa 1-0 na Mbeya City, Sokoine (TPL - 27/02/2019)

Timu ya Singida United imeendelea kuangusha pointi baada ya leo kukubali kichapo cha bao 1-0 kutoka kwa Mbeya City katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliopigwa kwenye Uwanja wa Sokoine Jijini Mbeya. Bao pekee la Mbeya City limefungwa na Iddy Selemani ‘Naldo’ dakika ya 55 akimalizia mpira ulioguswa na Mohamed Samatta kufuatia krosi ya Kenny Kunambi kutoka winga ya kulia. Matokeo hayo yameifanya Mbeya City ifikishe pointi 33 na kupanda kwa nafasi sita, kutoka nafasi ya 16 hadi nafasi ya 10 huku Singida United wakisalia katika nafasi ya 18 na pointi 29. Hili hapa goli la Mbeya City.