Content removal request!


Taifa Stars yarejea kutoka Uganda, Samatta asema bao alilokosa limemnyima usingizi

Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) imerejea leo Jijini Dar es Salaam kutoka nchini Uganda ilikokuwa kwaajili ya mchezo wa kufuzu fainali za AFCON dhidi ya Uganda (The Cranes) mchezo uliochezwa jana Septemba 8, 2018 na kumalizika kwa suluhu. Mara baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Dar es Salaam, nahodha wa timu hiyo Mbwana Samata, amesema hajapata usingizi baada ya kukosa goli la wazi kwenye mchezo huo huku akiwaomba radhi Watanzania. Katika mchezo huo, Samatta akiwa yeye na mlinda mlango Denis Onyango alikosa nafasi hiyo muhimu kwa Taifa Stars mchezo ukimalizika kwa suluhu. Mbali na Samatta, wachezaji wengine pia wa timu hiyo wamezungumza akiwemo Hassan Kessy, Agrey Moris na Aishi Manula. Naye kocha wa timu hiyo Emmanuel Amunike amewapongeza wachezaji kwa kucheza vizuri. Wakati huohuo Timu ya Taifa ya Lesotho imelazimishwa sare ya goli 1-1 dhidi ya timu ya Taifa ya Cape Verde katika mchezo uliochezwa Jumapili hii huko Maseru nchini Lesotho Matokeo hayo yametoa nafuu kwa Taifa Stars ambayo ipo kundi moja na timu hizo. Kundi L linaongozwa na Uganda yenye point 4, wakifutiwa na Lesotho wenye point 2, Stars point 2 na Cape Verde wakiburuza mkia wakiwa na alama 1.