Timu ya Malindi imepata ushindi wake wa kwanza kwenye michuano ya Kombe la Mapinduzi inayoendelea visiwani Zanzibar kwa kuifunga Jamhuri mabao 2-0 katika mchezo uliopigwa kwenye Dimba la Amaan. Mabao ya Malindi yamefungwa na Abdulswamad Ali dakika ya 17 na Juma Hamad dakika ya 62.