Content removal request!


ALLIANCE FC 0-2 SIMBA SC: HIGHLIGHTS & INTERVIEWS (TPL - 23/4/2019)

Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Tanzania bara Simba SC wamepata ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Alliance katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliopigwa leo kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza. Magoli ya Simba yamefungwa Haruna Niyonzima dakika ya 21 akimalizia krosi ya Mzamiru Yassin na Emmanuel Okwi dakika ya 75 baada ya kuichambua safu ya ulinzi ya Alliance kutokana na pasi safi ya Nicholas Gyan. Kwa matokeo hao, Simba inafikisha pointi 63 ikisalia kwenye nafasi ya tatu nyuma ya Azam FC yenye pointi 66 huku Yanga ikiwa kileleni na pointi 74 wakati Alliance FC ikirejea hatarini tena kwa kusalia katika nafasi yake ya 16 na pointi 37. Ushindi huo unarejesha matumaini kwa Simba katika mbio zake za kutetea taji lake baada ya kupoteza mchezo wake uliopita dhidi ya Kagera Sugar mjini Bukoba, na sasa inajiandaa kwa mchezo ujao dhidi ya Alliance FC utakaopigwa Aprili 25, 2019 kwenye uwanja huo huo wa CCM Kirumba jijini Mwanza.