Content removal request!


SIMBA SC 2-1 MTIBWA SUGAR: HIGHLIGHTS & INTERVIEWS (VPL - 13/9/2019)

Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara Simba SC wamepata ushindi wa pili mfululizo kwenye Ligi Kuu Tanzania Bara wakiichapa Mtibwa Sugar mabao 2-1 kwenye Dimba la Uhuru Dar es Salaam. Mabao ya Simba yamefungwa na Medie Kagere dakika ya 18 na Miraji Athuman dakika ya 69 huku bao pekee la Mtibwa likifungwa na Riphat Khamis Msuya dakika 21. Ushindi huo unaifanya Simba kufikisha pointi 6 kileleni baada ya kushindi mchezo wake wa kwanza kwenye Uwanja huo wakiichapa JKT mabao 3-1.