Content removal request!


Bao la Coastal Union: Mbao FC 0-1 Coastal Union (TPL - 11/02/2019)

Coastal Union imefanikiwa kuchukua pointi tatu ugenini kwa kuichapa Mbao FC bao 1-0 katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliopigwa kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza. Licha ya Mbao kumiliki zaidi mpira na kufanya mashambulizi mengi langoni kwa Coastal, nafasi pekee aliyoipata Raizin Hafidh dakika ya 60 aliitumia na kuipatia Coastal bao pekee lililoipa alama tatu ugenini.