SIMBA SC 8-1 COASTAL UNION: Timu ya Simba hii leo imepanda hadi nafasi ya kwanza kwenye msimamo ligi kuu soka Tanzania bara baada ya kupata ushindi wa bao 8-1 dhidi ya Coastal Union kwenye mchezo uliochezwa katika uwanja wa uhuru jijini Dar es Salaaam. Huu ni mshindi mkubwa zaidi katika ligi baada ya muda mrefu lakini rekodi mpya imeandikwa kwa wachezaji wawili wa timu moja katupia Hat-trick. Emmanuel Okwi amefunga magoli matatu na kumfanya afikishe mabao 14 msimu huu, wakati Hat-trick nyingine ya Meddie Kagere imemuongezea kasi kwenye msimamo wa wafungaji akifikisha mabao 20 kileleni akiwazidi wanaomfuatia kwa mabao manne. Mabao mengine ya Simba kwenye mchezo wa leo yamefungwa na Hassan Dilunga pamoja na Clatous Chama wakati lile la kufuatia machozi kwa Coast likifungwa na Raizin Hafidh