Kocha Msaidizi wa Simba SC ambaye anaiongoza timu hiyo katika michuano ya ligi ya Mabingwa Afrika, Thierry Hitimana, amezungumzia maandalizi yao kuelekea kuivaa Jwaneng Galaxy ya Botswana Jumapili Oktoba 24, 2021, uwanja wa Benjamin Mkapa kwenye mechi ya marudiano ya ligi ya Mabingwa Afrika. Simba inahitaji sare au ushindi ili kutinga hatua ya makundi ya ligi ya Mabingwa Afrika kutokana na ushindi wa 2-0 ugenini waliopata Oktoba 17, 2021 uwanja wa Taifa wa Botswana. #SimbaSC #JwanengGalaxy #ThierryHitimana #MpenjaTV