Content removal request!


GOLI & PENATI: TOWNSHIP ROLLERS 0-1 YANGA SC (CAF CL - 24/8/2019)

Timu ya Yanga SC imefanikiwa kusonga mbele na kuingia raundi ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa barani Afrika (CAF CL) ikiitupa nje Township Rollers ya Botswana kwa jumla ya mabao 2-1. Yanga imekamilisha ushindi huo kwenye mchezo wa marudiano wa raundi ya awali uliopigwa leo kwenye Dimba la Taifa la Botswana, ikishinda bao 1-0 lililofungwa na Juma Balinya dakika ya 42 kwa mpira wa ‘free-kick’. Katika mchezo huo, kipa wa Yanga Metacha Mnata ameibuka shujaa kwa kufuta penati ya Towship Rollers iliyopatikana dakika ya 66 baada ya mchezaji wake kuchezewa madhambi ndani ya eneo la hatari. Katika mchezo wa kwanza uliopigwa wiki mbili zilizopita, timu hizo zilitoka sare ya bao 1-1 kwenye Dimba la Taifa Dar es Salaam, Yanga ikisawazisha kwa penati kupitia kwa Patrick Sibomana baada ya kutanguliwa. Baada ya kufanikiwa kupenya katika hatua hiyo, sasa mabingwa hao wa kihistoria wa Tanzania Bara huenda wakakutana na Zesco ya Zambia inayonolewa na kocha wake wa zamani George Lwandamina. Zesco ambao leo wanarudiana na Green Mamba, wana nafasi kubwa ya kufuzu kwani tayari walishajiwekea kibindoni mabao 2-0 ugenini.