Meneja habari na mawasiliano wa Yanga SC Ally Kamwe hii leo kupitia Mpenja Tv, Amefunguka kuhusu maandalizi ya michezo yao ya Ligi ya Mabingwa Afrika ambapo Novemba 24 wataanzia nchini Algeria Dhidi ya CR Belouizdad. Ally Kamwe amesema kwamba kuelekea mchezo wao wa Disemba 2 dhidi ya Al Ahly wamejipanga kuhakikisha wanajaza uwanja mapema na kuleta burudani za kutosha siku ya mchezo huo.