Timu ya Biashara United ya Mara Jumamosi hii (Septemba 22, 2018) ilitoshana nguvu kwa kutoka suluhu dhidi ya JKT Tanzania kutoka Dar es Salaam. Mchezo huo wa Ligi Kuu Tanzania Bara ulipigwa kwenye dimba la Karume mjini Musoma, ambapo baada ya mchezo kocha wa Biashara United Hitimana Thiery ameonsha kutofurahia matokeo huku Bakari Shime kocha wa JKT akirishwa na matokeo hayo, na kusema yanamfanya ajiandae vyema na mchezo wake unaofuata dhidi ya Yanga. Nao Mashabiki wa Biashara United waliokuwepo dimbani hapo wakatoa maoni yao, wengi wakionesha kutorishwa na matokeo ya suluhu inayopata Biashara United katika mechi zake za nyumbani.