Content removal request!


Simba yaitafuna Mwadui 2-1 Kombe la Shirikisho (ASFC); Tazama magoli yote hapa

Wekundu wa Msimbazi Simba SC wamefanikiwa kutinga raundi ya tano (16 bora) katika michuano ya Kombe la Shirikisho la Azam Sports (ASFC) baada ya kuifunga Mwadui FC mabao 2-1 katika mchezo uliopigwa leo (25/01/2020) kwenye Uwanja wa Taifa Dar es Salaam. Mwadui ndiyo waliotangulia kupata bao kupitia kwa Gerald Mathias Mdamu dakika ya 35 kabla ya Clatous Chama kusawazisha dakika ya 45+2 na Francis Kahata kupiga la pili dakika ya 85.