Content removal request!


JKT TANZANIA 1-3 SIMBA SC: HIGHLIGHTS & INTERVIEW (VPL - 29/08/2019)

Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara Simba SC wameanza vema harakati za kulitetea taji hilo kwa kuichapa JKT Tanzania mabao 3-1 kwenye Dimba la Uhuru jijini Dar es Salaam. Mabao ya Simba kwenye mchezo huo yamefungwa na Medie Kagere aliyefunga mawili dakika ya 2 na 59, pamoja na Miraji Athuman dakika ya 74 huku Edward Songo akiifungia JKT bao pekee dakika ya 87. Mara baada ya mchezo, beki wa JKT Michael Aidan amesema kilichowamaliza nguvu ni bao la mapema la Simba ambalo limefanya wabadili mipango waliyoingia nayo. Kwa upande wake Nahodha wa Simba kwenye mchezo wa leo Mohamed Hussein akikiri kuwa kwa sasa morali ndani ya kikosi hicho iko chini lakini amewapongeza wachezaji wenzake kwa ushindi kwani utasaidia kupandisha ari ya kikosi. Baada ya kumalizika kwa raundi ya kwanza, Simba inakamata nafasi ya pili nyuma ya Lipuli FC na mbele ya Kagera Sugar, timu zote zikiwa na pointi tatu huku tofauti ya magoli ya kufunga na kufungwa ikiwa ni mbili.