Content removal request!


APR FC 1-0 PROLINE FC: HIGHLIGHTS (CECAFA KAGAME CUP - 6/7/2019)

Michuano ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati (CECAFA Kagame Cup) imeanza rasmi leo jijini Kigali nchini Rwanda kwa kushuhudia mechi mbili za Kundi C zikipigwa. Mchezo wa pili ambao ndiyo uliokuwa rasmi wa ufunguzi umeshuhudia vigogo APR kutoka Rwanda wakiwatandika Proline FC kutoka Uganda bao 1-0. Bao la APR limefungwa kunako sekunde ya mwisho kabisa ya mchezo dakika ya 90+4 ukitokana na mpira wa free-kick uliogonga mwamba na kukutana na Manzi Thierry aliyeihakikishia APR pointi tatu muhimu.