Mabingwa wa kihistoria wa Ligi Kuu Tanzania Bara wameendeleza ‘unyama’ nje ya Jiji la Dar es Salaam baada ya leo kuichapa Kagera Sugar mabao 2-1, mchezo ukipigwa kwenye Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba. Mabao yote ya Yanga yamefungwa kwa kichwa, la kwanza likifungwa na Heritier Makambo dakika ya 21 na la pili likifungwa na Raphael Daud aliyeingia kutokea benchi dakika ya 74 huku bao la Kagera Sugar likifungwa na Ramadhan Kapera kwa mkwaju wa penati dakika ya 32. Huu ni mchezo wa pili kwa Yanga kupata ushindi nje ya Dar es Salaam baada ya kuichapa Mwadui FC mabao 2-1 Novemba 21 mjini Shinyanga na pia ni ushindi wao wa 10 katika mechi 12 ambazo wamecheza msimu huu huku wakiendeleza rekodi yao ya kutopoteza mchezo wowote hadi sasa. Haya hapa magoli yote ya mchezo huu.