Coastal Union ya Jijini Tanga imeshindwa kufurukuta katika dimba lake la nyumbani, Mkwakwani, baada ya kulazimishwa sare ya bao 1-1 na Lipuli FC kwenye mchezo wa kwanza la Ligi Kuu Tanzania msimu huu. Wageni Lipuli FC ndiyo waliotangulia kupata bao dakika ya 59 kupitia kwa Zawadi Mauya na dakika kumi baadaye Coastal wakasawazisha kupitia kwa Bakar Mwamnyeto dakika ya 69. Haya hapa mabao yenyewe.