Content removal request!


Mashabiki Simba wamkosoa kocha wao baada ya kuchapwa 2-1 na Nkana FC

Mabingwa wa Tanzania Bara Simba SC wamepoteza mchezo wao wa kwanza wa raundi ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa Barani Afrika (CAF CL) kwa kipigo cha mabao 2-1 kutoka kwa Mashetani Wekundu wa Nkana FC katika mchezo uliopigwa mjini Kitwe nchini Zambia. Baada ya mchezo huo, mashabiki wa Simba waliokuwa wakiufuatilia mchezo huo kupitia Azam TV wametoa maoni yao, huku wakiuchambua mchezo huo, na wengine wakimkosoa kocha wa timu hiyo Patrick Aussems.