Mbao FC imepata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Ruvu Shooting katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliopigwa leo kwenye uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza. Katika mchezo huo uliokuwa mkali, Mbao wamepata bao hilo dakika ya 33 kupitia kwa Raphael Siame dakika 33.