Ruvu Shooting na Mbeya Kwanza zimekabana koo na kutoka sare ya bao 1-1 katika mchezo wa #NBCPremierLeague ulipigwa leo kwenye Dimba la Benjamin Mkapa, Dar es Salaam. Sadat Mohamed Nanguo ndiye aliyetangulia kupachika bao upande wa Ruvu Shooting na kisha Habib Kiyombo akasawazisha kwa 'free-kick'