Yanga SC imeitandika Dodoma Jiji mabao 2-0 katika mchezo wa ligi kuu ya NBC Tanzania Bara uliopigwa leo mei 15, 2022 kwenye Uwanja wa Jamhuri, Dodoma. Magoli ya Yanga kwenye mchezo huu yamrfungwa na Dickson Ambundo dakika ya 13 na lingine la kujifunga kutoka kwa golikipa wa Dodoma Jiji, Mohamed Yusuph dakika ya 35. Katika mchezo huo pia Dodoma Jiji wamepata pigo kwa kiungo wao Hassan Nassor Maulid kutolewa nje kwa kadi nyekundu baada ya kumchezea rafu kiungo wa Yanga, Yannick Bangala.