Content removal request!


MAGOLI YOTE SITA: MWADUI FC 3-3 MBAO FC (TPL - 14/05/2019)

Timu ya Mwadui FC ya mkoani Shinyanga imelazimishwa sare ya bao 3-3 na Mbao FC katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliopigwa leo kwenye Uwanja wa Mwadui Complex mkoani humo. Mbao FC ndiyo waliotangulia kupata mabao 2-0 hadi kipindi cha kwanza kinamalizika lakini wenye Mwadui wakapindua matokeo na kupata mabao matatu, kabla ya Mbao kurejea tena mchezoni na kusawazisha. Mabao ya Mbao FC yamfungwa na Abubakar Ngalema dakika ya 35, Said Hamis Jr dakika ya 44 na Hamim Abdulkarim dakika ya 86 wakati mabao ya Mwadui yakifungwa na Leonard Bhoke dakika ya 46, Gerard Mathias Mdamu dakika ya 58 na Ottu Joseph dakika ya 69. Matokeo haya yanazifanya timu zote mbili kugawana pointi ambapo Mbao wamefikisha pointi 44 na kukaa nafasi ya kumi baada ya kucheza mechi 36 huku Mwadui wakifikisha pointi 38 katika mechi 36 na kusalia nafasi ya 19.