Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Simba SC wameangukia pua kwa kichapo cha bao 1-0 kutoka kwa Mbeya City, mechi ikipigwa kwenye Dimba la Sokoine jijini Mbeya. Goli pekee la Mbeya City limefungwa na Paul Nonga huku Mbeya City wakipata pigo kwa beki wake Mpoki Mwakinyuke kutolewa kwa kadi nyekundu na Simba wakikosa penati iliyopigwa kwa Chris Mugalu.