Content removal request!


UCHAMBUZI: Kilichoipa Simba ushindi dhidi ya Nkana FC CAF CL (DAKIKA 90 – 24/12/2018)

Sehemu ya kwanza ya kipindi hiki imechambua kwa kina mchezo wa marudiano wa Ligi ya Mabingwa Afrika kati ya Simba SC dhidi ya Nkana FC uliopigwa kwenye Uwanja wa Taifa Dar es Salaam, na Simba kupata ushindi wa mabao 3-1. Ushindi huo uliifanya Simba iweze kufuzu hatua ya makundi ya michuano hiyo kwa mara ya kwanza baada ya miaka 15 kutokana na ushindi wa jumla wa mabao 4-3 kufuatia kipigo cha mabao 2-1 ilichokipata nchini Zambia kwenye mchezo wa kwanza. Je, nini sisi ya ushindi huu? Kutana na wachambuzi wetu ni Abdullah Mkeyenge, Charles Abel na Thobias Sebastian, chini ya Ahmed Ally. Mbali na hilo, kipindi hiki pia kimechambua mechi za Kombe la Shirikisho la Azam Sports ikiwemo ile ya Yanga kushinda mabao 4-0 dhidi ya Tukuyu Stars kwenye Dimba la Taifa Dar es Salaam. Sehemu ya mwisho ya kipindi hiki tunaangazia Ligi Daraja la Kwanza, leo tukijikita zaidi kwenye viwango na mafanikio ya timu za Daraja la Kwanza kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho la Azam Sports. Kumbuka kipindi cha Dakika 90 ni kila Jumatatu saa 3:30 usiku, Azam Sports 2.