Simba SC imeibuka na ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya Namungo FC katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliopigwa usiku wa leo 29/02/2020 kwenye Dimba la Taifa Dar es Salaam. Mabao ya Simba yamefungwa na Francis Kahata dakika ya 22, Hassan Dilunga dakika ya 39 na Medie Kagere dakika ya 89 huku Namungo ikijipatia magoli yake kupitia kwa Bigirimana Blaise dakika ya 35 na Lucas Kikoti dakika ya 72.