HISTORIA IMEANDIKWA DODOMA Ni historia tangu kuzaliwa kwa taifa la Tanzania mechi ya ligi kuu kuoneshwa usiku kutoka jijini Dodoma baada ya Uwanja wa Jamhuri kuwekwa taa. Ilikuwa ni Dar es Salaam na Zanzibar pekee ambako kuna viwanja vyenye taa zinazofaa kuonesha mpira ‘LIVE’ wakati wa usiku, lakini kuanzia sasa, Dodoma nayo imeongezeka ikiwa ni kwa udhamini wa Azam TV. Mechi ya kwanza kabisa kuwa sehemu ya historia hii imewakutanisha wenyeji Dodoma Jiji FC dhidi ya Tanzania Prisons kutoka mkoani Rukwa na kushuhudia ‘Wajelajela’ wakiliwa kwa kichapo cha mabao 2-1. Azam TV imezidi kuongeza wigo wa burudani ya soka kwenye TV kwa nyakati tofauti usiku na mchana na huu ni mwanzo tu. Magoli ya Dodoma Jiji yamefungwa na Khamis Mcha kwa penati pamoja na Emmanuel Martin wakati Tanzania Prisons walianza kupata bao kupitia kwa Jeremiah Juma. Tufuatilie kwenye mitandao mingine ya kijamii:- ►INSTAGRAM: https://www.instagram.com/azamtvtz/ ►INSTAGRAM: https://www.instagram.com/azamsports2/ ►TWITTER: https://twitter.com/azamtvtz ►FACEBOOK: http://www.facebook.com/azamtvtz ►WEBSITE: http://www.azamtv.co.tz