Timu ya Biashara United kutoka mkoani Mara imepata sare ya bao 1-1 dhidi ya mabingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara Simba SC katika mchezo uliopigwa leo kwenye Dimba la Taifa Dar es Salaam. Biashara ndiyo waliotangulia kupata bao kupitia kwa Innocent Edwin dakika ya 14 kabla ya Simba kusawazisha dakika ya 17 kupitia kwa Clatous Chama akimalizia krosi ya Mohamed Hussein. Sima imefikisha pointi 92 kileleni wakati Biashara United ikifufua matumaini ya kubaki ligi kuu kwa kujiongeza pointi moja na kufikisha pointi 44 kwenye nafasi ya 12. Katika mchezo wa mwisho Biashara itacheza ugenini dhidi ya Mbeya City na italazimika kushinda au kupata sare ili kuepuka adhabu ya kushuka daraja moja kwa moja wakati Simba ambayo haina cha kupoteza ikienda kumalizia mkoani Morogoro dhidi ya Mtibwa Sugar na kukabidhiwa kombe lao la ubingwa.