Hatimaye Ihefu SC wamevunja mwiko wa Yanga kutopoteza mchezo katika mechi 49, wakiwatandika 2-1 kwenye Uwanja wa Highland Estate, Mbarali mkoani Mbeya. Yanga wametangulia kwa goli la Yanick Bangala dakikaya 9, kabla ya Never Tigere kusawazisha kwa free-kick dakika ya 39... Lakini Lenny Kissu akafunga kona iliyopigwa na Never Tigere dakika ya 62. Mara ya mwisho Yanga kupoteza mchezo wa ligi kuu ilikuwa ni Aprili 25, 2022.