Namungo FC imeitandika Ruvu Shooting mabao 3-1 katika mchezo wa ligi kuu ya NBC Tanzania Bara uliochezwa Aprili 18, 2022 kwenye Uwanja wa Ilulu mkoani Lindi. Katika mchezo huo, David Molinga amefunga goli lake la kwanza kabisa kwenye ligi msimu huu, huku mengine yakifungwa na Hashim Manyanya pamoja na Emmanuel Charles wakati goli la kufutia machozi likifungwa na Sadat Mohamed Nanguo.