Timu ya Mtibwa Sugar imeendelea kupokea vipigo kwenye Ligi Kuu Tanzania Bara baada ya leo kufungwa mabao 2-1 na Biashara United kwenye Uwanja wa Karume mjini Musoma. Wenyeji Biashara United ndiyo waliotangulia kupata bao dakika ya 39 kupitia kwa George Makang’a kwa mpira wa adhabu ndogo ‘free-kick’, lakini Mtibwa walisawazisha kupitia kwa kichwa cha Riphat Kamis dakika ya 64 na kisha Biashara kupata bao la ushindi dakika ya 80 kupitia kwa Innocent Edwin.