Content removal request!


Coastal Union ilivyojipanga kutoshuka daraja, kamati ya usajili yamwaga mikakati

Siku chache baada ya ratiba ya msimu ujao wa Ligi Kuu Tanzania Bara kuwekwa hadharani, Klabu ya Coastal Union ya Tanga imesema imeweka mikakati kabambe ya kufanya vizuri. Ikiwa imerejea katika ligi baada ya kuikosa msimu uliopita, uongozi wa Coastal Union umesema upo katika mikakati mizito kuhakikisha timu hiyo inafanya vizuri katika msimu ujao wa ligi hiyo. Timu hiyo inayotumia Uwanja wa Mkwakwani uliopo Tanga kama uwanja wake wa nyumbani, katika msimu ujao wa ligi kuu imepangwa kufungua dimba na Lipuli FC ya Iringa Agosti 22, mwaka huu mjini Tanga. Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Coastal Union, Steven Mguto, amesema kamwe safari hii hawatakubali kushindwa na kushuka tena daraja kwenda kucheza Ligi Daraja la Kwanza.