Msafara wa timu ya Simba umewasili salama nchini Algeria Jumatano Machi 6, tayari kwaajili ya mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya JS Saoura ya nchini humo. Mara baaa ya kuwasili katika mji wa Algers, kikosi hicho kimefanya mazoezi mepesi katika Uwanja wa Ben Siam ambao ni uwanja wa mazozi wa timu ya ligi kuu ya Algeria ya 'NA Hussein-Dey' kabla ya kuifuata Saoura katika mchezo utakaopigwa Jumamosi, Machi 9. 2019. Afisa Mtendaji Mkuu wa timu hiyo Crescentius Magori pamoja na Naohodha John Bocco wameeleza mikakati ya timu hiyo huku Balozi wa Tanzania Yusuph Omar Mzee akitoa tahadhari na mkuu wa msafara Ahmed Mgoyi ambaye ni Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya TFF akazungumzia ushirikiano kutoka TFF kuhakikisha Simba imafanikiwa kwenye michuano