Timu ya taifa ya Burundi imekuwa ya kwanza kuaga mashindano ya CECAFA Challenge Cup baada ya leo kupoteza mchezo wa tatu mfululizo, ikifungwa na 2-1 na Djibouti. Magoli ya Djibouti yamefungwa na Mahdi Hussein dakika ya 11 na 71 huku bao pekee la Burundi likifungwa na Ndikumana Laundry dakika ya 14. Matokeo hayo yanaifanya Burundi kupoteza mechi zote tatu huku ikibakiza mchezo mmoja ambao hata ikishinda, haitaweza kusonga mbele ikiwa ndiyo timu pekee isiyokuwa na pointi kati ya timu tano za Kundi A.