Azam FC imeendelea kuangusha pointi baada ya leo kubanwa na Coastal Union kwa kulazimishwa sare ya bao 1-1 katika mchezo wa Ligi kuu Tanzania Bara uliopigwa kwenye Uwanja wa Mkwakwani Jijini Tanga. Wenyeji Coastal Union ndiyo waliotangulia kupata bao dakika ya 45+2 kupitia kwa Ayoub Lyanga, lakini Obrey Chirwa akasawazisha bao hilo dakika ya 51 ya mchezo. Azam sasa wamefikisha pointi 50 katika nafasi ya pili baada ya kucheza mechi 24 huku Coastal wakiwa nafasi ya saba na pointi 34 baada ya kucheza michezo 26.