Content removal request!


Azam yalazimishwa sare ya 1-1 na Mtibwa, kadi mbili nyekundu zatoka

Azam FC, imepata alama moja kwenye sare ya bao 1-1 dhidi ya Mtibwa Sugar katika mchezo huo wa Ligi Kuu Tanzania Bara (VPL) uliochezwa leo jioni Uwanja wa Taifa Dar es Salaam. Ismail Aidan Mhesa, aliwatanguliza Mtibwa Sugar, kabla ya Azam FC kusawazisha kupitia kwa Richard Djodi aliyefunga kwa mkwaju wa penati.