Content removal request!


SIMBA SC 0-0 LIPULI FC; HIGHLIGHTS & INTERVIEWS (23/11/2018)

Ligi Kuu Soka Tanzania Bara imeendelea leo kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam ambapo mabingwa watetezi Simba wamelazimishwa suluhu na Lipuli FC kutoka mkoani Iringa. Mchezo huo uliokuwa mkali na wenye ushindani, ulitawaliwa na kosakosa kila upande ambapo Simba walipoteza nafasi zaidi ya nne kupitia kwa mshambuliaji wao John Bocco, huku Lipuli walipoteza nafasi takriban tatu walizopata kutokana na makossa ya beki wa Simba Paul Bukaba. Makosa ya beki huyo yalimlazimu kocha wa Simba kufanya mabadiliko kwa kumtoa na nafasi yake kuchukuliwa na James Kotei dakika ya 38 ya mchezo. Kunako dakika za nyongeza, Meddie Kagere alikuwa ameshatikisa nyavu za Wanapaluhengo Lipuli FC lakini kwa mujibu wa mwamuzi wa pembeni, ilikuwa ni 'off-side' hali iliyoonekana kuzua malalamiko kwa upande wa Simba. Mara baada ya mchezo Nahodha wa Simba John Bocco amesema kilichowakosesha ushindi ni kukosa bahati, huku Nahodha wa Lipuli Ally Mtoni akisema kuna mbinu ambazo wao huzitumia kila wanapokutana na timu kubwa ili kupata pointi. Matokeo hayo ambayo ni mwendelezo wa rekodi ya Kocha wa Lipuli Selemani Matola kutofungwa na Simba yameiacha Simba ibaki katika nafasi ya tatu ikiwa na alama 27 baada ya kucheza mechi 12.