Polisi Tanzania imeizuia Simba kufunga goli hata moja kwenye mchezo wa ligi kuu ya NBC Tanzania Bara uliochezwa leo kwenye Dimba la Ushirika, Moshi na kufanya matokeo yawe 0-0. Hii ni mara ya kwanza kwa Polisi Tanzania kupata angalau alama moja mbele ya Simba tangu ipande daraja msimu wa 2019/20. Tazama baadhi ya matukio kutoka kwenye mchezo huo.