Kagera Sugar imeendeleza ubabe kwa kushinda mchezo wa tatu mfululizo kwenye ligi kuu baada ya leo kuitandika Coastal Union mabao 2-1 kwenye Dimba la Kaitaba mjini Bukoba. Eric Mwijage ndiye aliyefunga magoli yote mawili ya Kagera Sugar huku Vicent Abubakary Vicent akifunga goli pekee la Coastal Union.