Content removal request!


Magoli yote Yanga ikiichakaza Rhino Rangers 7-0 Azam Sports Federation Cup 29/01/2023

Yamefungwa magoli saba, yote yakitoka Yanga dhidi ya Rhino Rangers kutoka Ligi Daraja la Pili, katika mchezo wa kusaka kuingia hatua ya 16 bora, Azam Sports Federation Cup uliopigwa kwenye Dimba la Benjamin Mkapa, Dar es Salaam. Kennedy Musonda amefunga magoli mawili dakika ya 16 na 46 huku mengine yakitoka kwa Dickson Ambundo dakika ya 7, Stephane Aziz Ki dakika ya 20, Farid Mussa dakika ya 25, Yannick Bangala dakika ya 26 na David Bryson dakika ya 90'+3. Kwa ushindi huu, Yanga sasa itakipiga dhidi ya Tanzania Prisons katika hatua ya 16 bora.