Content removal request!


MAGOLI: MTIBWA SUGAR 4-0 NORTHERN DYANAMO (CAF Conf. Cup - 27/11/2018)

Timu ya Mtibwa Sugar ya mkoani Morogoro imeanza vyema michuano ya Afrika kwa kuichapa Northern Dynamo mabao 4-0 katika mchezo wa hatua ya awali wa Kombe la Shirikisho barani Afrika. Katika mchezo huo uliopigwa kwenye Dimba la Azam Complex Chamazi, mshambuliaji wa Mtibwa Jaffary Salum Kibaya ameibuka shujaa kwa kupigwa hat-trick, akifunga mabao yake katika dakika za 13, 36 na 58 huku bao la nne likifungwa na Riphat Khamis aliyeingia kipindi cha pili kuchukua nafasi ya Ismail Mhesa. Kwa matokeo haya, mtibwa wamejiweka pazuri katika njia kusonga mbele kwani watahitaji sare ya aina yoyote ili kufuzu hatua inayofuata au wasifungwe mabao zaidi ya matatu.