Dodoma Jiji na Biashara United zimeumana na kutoka sare ya bao 1-1 katika mchezo mkali wa #NBCPremierLeague uliochezwa leo kwenye Dimba la Jamhuri, Dodoma. Dodoma Jiji wameanza kupata bao lao dakika ya 10 kupitia kwa Anuary Jabir na Biashara kusawazisha dakika ya 63 kupitia kwa Deogratius Mafie.