Content removal request!


Goli: Alliance FC 'yawatungua' 1-0 maafande wa JKT Tanzania (TPL - 21/02/2019)

Alliance FC ya jijini Mwanza imeendeleza rekodi yake ya kutopoteza mchezo kwenye uwanja wake wa nyumbani wa Nyamagana baada ya leo kuichapa JKT Tanzania bao 1-0 katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara (TPL). Bao pekee la Alliance limefungwa na Bigirimana Blaise akimalizia kwa kichwa mpira ulipigwa kwa kichwa na Dickson Ambundo dakika ya 29.