Wenyeji Uganda wamefuzu nusu fainali baada ya kushinda mchezo wake wa tatu mfululizo, ikiichapa Ertitrea mabao 2-0. Magoli ya Uganda yamefungwa na Nicholas Kazozi dakika ya 57 pamoja na Mustafa Kizza kwa mkwaju wa penati dakika ya 79. Matokeo hayo yanaifanya Uganda kuongoza kundi A ikiwa na pointi tisa, ikifuatiwa na Djibouti yenye pointi 4, Eritrea pointi 3, Somalia nafasi ya nne na pointi 1 na mkiani wapo Burundi wakiwa hawana pointi.