Content removal request!


MAGOLI: TZ PRISONS 2-1 MBAO FC - Kocha wa Mbao asingizia uwanja (TPL – 06/02/2019)

Tanzania Prisons imepata ushindi wa mabao 2-1 katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliopigwa Februari 6, 2019 kwenye Uwanja wa Sokoine Jijini Mbeya. Magoli ya Wenyeji hao wa mchezo yamefungwa na Salum kKimenya dakika ya 12 na Adam Adam dakika ya 20 huku Mbao wakipata bao lao kwa mpira wa adhabu ndogo dakika ya 34 kupitia kwa Amosi Charles. Baada ya mchezo huo makocha wa timu zote mbili wakazungumza ambapo Kocha wa Tanzania Prisons Adolf Rishard amewapongeza wachezaji wake wa ushindi huku akitaja mvua kuwa kikwazo kwa upande wao, wao kocha wa Mbao FC Ally Bushiri akilalamikia hali ya uwanja kuwa sababu ya wao kupoteza mchezo. Tazama magoli na mahojiano