Content removal request!


JKT TANZANIA 1-1 ALLIANCE FC; HIGHLIGHTS & INTERVIEWS (07/10/2018)

JKT Tanzania leo wamebanwa mbavu na Alliance ya Mwanza kwa kulazimishwa sare ya bao 1-1 katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliopigwa kwenye Uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo Jijini Dar es Salaam. Wenyeji JKT ndiyo waliokuwa wa kwanza kupata bao kwa mpira wa ‘free-kick’ kupitia kwa Abdulrahman Mussa dakika ya 70 kabla ya Alliance kusawazisha dakika ya 90 kupitia kwa Juhudi Philimon aliyeingia kipindi cha pili.