Kagera Sugar wamefanikiwa kusalia ligi kuu baada ya kuwafunga Pamba magoli 2-0 katika mchezo uliochezwa kwenye uwanja wa Kaitaba mkoani Kagera. Ally Ramadhan na Japhet Makalai ndiyo mashujaa wa Kagera ndiyo waliokuwa mashujaa kwani yao ya dakika ya 51 na 79 ndiyo yaliyoibakiza timu hiyo kwenye ligi kuu msimu ujao. Akizungumza kwa kujiamini kocha wa Kagera Sugar Mecky Mexime amesema alijua kuwa timu yake ingebaki ligi kuu na kwamba hakua na hofu hata kidogo, wakati kocha wa Pamba Ali Omar Kisaka yeye amesema vijana wameshindwa kutumia nafasi.