Content removal request!


TANZANIA U-23 (3-1) BURUNDI U-23: FULL HIGHLIGHTS

Mchezo wa raundi ya pili wa kuwania kufuzu kwa michuano ya Afcon kwa vijana wa U-23 kati ya Tanzania na Burundi uliopigwa kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Tanzania ilishinda kwa mabao 3-1 lakini hata hivyo imeondolewa kwenye michuano hiyo licha ya matokeo ya jumla kuwa 3-3. Burundi imenufaika kwa faida ya bao la ugenini baada ya kushinda kwa mabao 2-0 kwenye mchezo wa kwanza uliochezwa jijini Bujumbura. Magoli ya Tanzania kwenye mchezo huo yalifungwa na Habib Kyombo, Mbaraka Yusuph na Salum Kihimbwa.