Content removal request!


Mazoezi na safari ya Simba kutoka Algers hadi Bechar kuifuata JS Saoura. Kocha azungumza

Kikosi cha Simba usiku wa jana (Machi 7, 2019) kilifanya mazoezi ya mwisho kwenye mji wa Algeria, ikiwa ni kipindi chake cha pili cha mazoezi tangu kuwasili nchini Algeria, safari hii kikitumia Uwanja unaomilikiwa na Kituo cha Zimamoto cha Algiers. Leo asubuhi (Machi 8, 2019) kimeanza safari ya kutoka Algers kwa ndege, kuelekea katika Mji wa Bechar ambako ndiko mchezo wao dhidi ya JS saoura utapigwa. Kabla ya safari, Kocha Mkuu wa timu hiyo Patrick Aussems alizungumza na Azam TV kuhusu mechi hiyo na kugusia urefu wa safari, mbinu atakazotumia kucheza na JS Saoura pamoja na hali ya hewa waliyokutana nayo.