Kocha mkuu wa Biashara United Amri Said ametoa ufafanuzi juu ya sakata la mlinda mlango wake Nouridine Balora ambaye walipishana kauli wakati wa mchezo wa raundi ya nne ya Kombe la Shirikisho la Azam Sports walipokuwa wakicheza dhidi ya Yanga. Amri Said amesema kuwa balora alifanya kitendo cha utovu wa nidhamu baada ya kufanyiwa mabadiliko kwenye mchezo huo ambapo, wakati anaelekea kwenye benchi alikuwa akiongea maneno ambayo si mazuri kama mchezaji. Katika mchezo huyo Yanga ilishinda kwa penati 5-4 baada ya sare ya mabao 2-2.