Content removal request!


FULL HIGHLIGHTS: MBEYA CITY 0-0 JKT TANZANIA (TPL – 08/11/2018)

Maafande wa JKT Tanzania wamewalazimisha suluhu vijana wa Mbeya City katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliopigwa leo kwenye Uwanja wa Sokoine, Jijini Mbeya. Tazama hali halisi ilivyokuwa pamoja na highlights za mchezo wenyewe. Katika mchezo huo JKT walionekana kuwa moto zaidi hasa kipindi cha kwanza kwa kutengeneza mashambulizi kadhaa na kupoteza nafasi takriban tatu lakini kipindi cha pili timu zote zilikuwa zikishambuliana kwa kushtukiza. Hata hivyo mchezo huo ulichelewa kuanza kwa takriban dakika ya 20 kutokana na maandalizi ya uwanja kutokamilika kwa wakati kwani hadi inatimia saa 10:00 jioni uwanja ulikuwa bao haujachorwa alama, jambo ambalo baadaye lilifanywa na vijana wa kuokota mipira.